NASH EMCEE
Friday, May 1, 2015
KISWAHILI NA SANAA – MZIMU WA SHAABAN ROBERT.
Tuesday, April 21, 2015
HAKIKA "BAADA YA CHUO" HUAKISI MAISHA YA WASOMI WENGI.
Angalia: Kibao nambari 04. |
Wednesday, April 15, 2015
NASH MC: AJA TENA NA PICHA JONGEFU YA WIMBO " HASI 15 ".
Nash Mc. |
NASH MC: "ZIARA YA KINASA BADO INAENDELEA".
Sunday, September 7, 2014
UNAKIJUA KIBAO CHA " MSHAIRI " KUTOKA KATIKA EP YA MCHOCHEZI ?
JE! UNAKIJUA KIBAO CHA " MSHAIRI " KUTOKA KATIKA EP YA MCHOCHEZI ?
Karibuni wapenzi wafuatiliaji wa blogu hii makini kabisa, leo kuna swali juu yako wewe shabiki wa Nash Mc, swali kama linavyosomeka hapo juu, je unamfahamu vipi NASH MC?, je unaelewa mapito ya kimaisha aliyopitia?, sasa nakuibia siri kuwa kibao nambari 03 ndiyo jibu.
Fanya hivi sikiliza kibao hiko utagundua mengi juu yake, pata nakala yako ya MCHOCHEZI, sikiliza kibao kiitwacho mshairi, lakini ziada ni kuwa elimu, burudani kutoka vibao vingine vitakupa ile dhima ya kazi ya sanaa. sasa je, " hakuna anayetudai, sasa kwanini tusifurahiiii? ".
Na, Mwanazuoni (Mlela)/ Muendesha blogu |
Saturday, September 6, 2014
# NashMC TEMEKESHOW Inakaribia......
Baada ya kikosi kizima cha maandalizi ya Show hiyo kujipanga vyema, kinawakumbusha mashabiki wa kweli kukaa mkao wa kufurahi siku ya tumbuizo hilo mara tu tarehe na siku vikitajwa, wewe na yule hamtakiwi kukosa siku hiyo.
# NashMcTemekeShow inakaribia.....
Saturday, March 8, 2014
NASH MC ATOA TAARIFA KWA UMMA: KUHUSU SANAA NCHINI NA HALI HALISI YA MAPOKEO YA KIBAO "KAKA SUMA".
Monday, March 3, 2014
BAADA YA "NAANDIKA" SASA NASH EMCEE AJIAANDAA TOKA NA "EP".
Oi, oi, oi, kama ilivyoada utamaduni wa Hiphop unavyotulea katika misingi yake ELIMU NA BURUDANI, basi nasi hatuna budi kutomuangusha mlezi huyu, leo katika blogu letu makini kabisa, kuna hili, NASH MC, baada ya kuachia kibao chake "naandika",mwanzoni mwa mwaka huu na kupokelewa vizuri na wanajamii (Wapenzi wa HipHop. Sasa yuko jikoni akijiandaa kutoka na "EP", yaani "Extended Play", mmmh!, " EP", ndo, nini sasa?, waweza jiuliza ukabaki na uvulivuli katika hili, ila hapa tutaelezana, dhana hii inanikumbusha kipindi THORIA alivyoachia kazi zake zake za mwanzo kabisa katika mfumo huu, hivyo sasa "EP", ni demo album (santuri) yenye nusu nyimbo zitakazokua kwenye album(santuri) ni kama trailor tracks (vionjo) vya albam inayokuja, wakati mwingine watu wanatoa ili wawape mashabiki kitu cha kuwa weka katika umakini kabla album (santuri) kamili haijatoka, na inakuwa na nyimbo mpaka 7, hivyo sasa Nash anawaambia mashabiki wake wakae mkao wa kupata kazi hii, endelea kutembelea www.nasheemcee.blogspt.com, waambie na wale pia, HipHop Kwa Maisha.
Thursday, February 20, 2014
" NAANDIKA ", NI KIBAO KIPYA CHA HIPHOP MWANZONI MWA 2014, JE WAJUA KIMEBEBA MAUDHUI YAPI?, FUATILIA HAPA UJIFUNZE.
Mwanazuoni, 0654 30 40 30.
Wednesday, February 19, 2014
P THE MC NA " BORN TO RHYME NOT TO SHINE "..
YARUDI UPYA KWA MAARIFA KUHUSU HIPHOP, BIDHAA ZA WASANII WA HIPHOP, MAKALA/ CHAMBUZI MAKINI .
zetu (posts), mwambie mpenda HIPHOP yeyote wakweli juu ya hili, HABARI IFIKE MBALI.
Tuesday, September 24, 2013
Vibao vyao na mitambao yao vyote viliendelea chakatwa na ubongo wangu vyema na moja kwa moja vikanisanisafirisha mpaka kwenye kitabu maridhawa kabisa kuhusu utamaduni huu wa HIPHOP nikapenyeza kidole na kwenda kubisha hodi kwenye ukurasa ulioandikwa yaliyomo nao moja kwa moja ukanielekeza ukurasa wa 47 ambapo nilijazwa unene wa maarifa nilipogundua kuwa kilichozungumzwa hapo ni NGUZO ZA HIPHOP,ambapo hapo wengi walijimwaya na kutaja idadi ya NGUZO ZA HIPHOP mfano, TOVUTI YA URBAN DICTIONARY Ilitoa idadi ya nguzo kama tisa (9)kwa idadi yake kama Mcing,d-jaying,battlelling,graffiti,B-boying,Beat boxing,The style(fashion),The slang,rope skipping,pia hawa hawakubaki nyuma. WIKIPEDIA. Mtandao huu ulitoa hizi Mcing,d-jaying,break dance,na graffiti,beat boxing,lakini katika hizi Mwanaharakati AFRIKA BAMBATAA alizitaja zote kasoro beat boxing,sasa nkajiuliza JE KUNA NGUZO NGAPI ZA UTAMADUNI HUU? YOUTH ETHICS INITIATIVE INC kwa ushirikiano na CHUO KIKUU CHA MIAMI. Walisema kiasilia kulikuwa na nguzo nne (4) yaani Uchenguaji,umanju,uvunjaji,machata lakini nguzo ya tano ''Maarifa''ikaongezeka Swadkta kabisa kuangalia muda nikiwa safari nilijikuta nkigonga mlango (ukurasa) nambari 48 palipodadavuvuliwa nguzo ya maarifa kwa heshima kabisa nikaisoma na kuhitimisha katika kutafuta mengi pitia vyanzo mbalimbali nikazidi ingia ndani ya milango hiyo nikajikuta nikigonga mlango nambari 54,56 na 58.na kuwaleteeni haya. NANI ALIKUWA ''MC'' WA KWANZA? Ni swali zuri lakini wengi tunaopenda HipHop hatufahamu kama ni kweli,narudi palepele kwamba tafuta ufahamu/maarifa (Knowledge)kama mimi ninavyojaribu pindi panapopatikana upenyo ama muda,safi jibu la swali ni kwamba ingawa inaaminika kuwa COKE LA ROCK ndiye aliyekuwa mchenguaji wa kwanza wa HIPHOP lakini si wa kwanza kuanzisha neno ''MC''sasa. JE NANI ALIANZA TUMIA NENO HIPHOP? Ndiyo,swali mezani kama tulivyoona hapo juu kuwa Bw.Coke La Rock ndiye mgahanaji wa kwanza lakini hakulitumia neno ''MC''katika kujiita na kuliingiza katika utamaduni wa HipHop kwa kina lakini MELLE MEL huyu anageuka kinara wakuliingiza neno hili katika Hiphop,ndugu huyu aliyezaliwa huko South Bronx jijini New York,Marekani mwaka 1961,alileta athari kubwa katika utamaduni wa HIPHOP kwa kuleta mitindo mbalimbali ya ghani,Mchenguaji wa HipHop wa kwanza kupata tunzo ya Grammy,pia kibao chake kiitwacho ''The Message'' ndicho cha kwanza katika utamaduni wa HipHop kuingia katika kumbukumbu za taifa za vibao vya kihistoria (United States National Archive of Historic Recordings),toka katika hili ndipo laja hili. JE KWANINI NASH ALIJIITA ''MC''? Katika tafsiri zoefu neno ''Mc'' ni mchenguaji au mshereheshaji au kwa kimombo yaweza andikwa kama ''Master of ceremony''kwa maana ya kuwa muongoza hafla ama sherehe au tumbuizo,akhsante sidhani kama nimetukana katika hili lakini naamini kuwa majina yetu mengi tumerithi kwa wale tulowakuta kwa lengo la kuwaenzi au mapenzi yetu,hivyo kama mistari kadhaa hapo juu ilivyoeleza kuwa MELLE MEL ameacha athari ya mitambao mingi kwa wale waliomfatilia/mashabiki wake hivyo hata jina au neno ''MC'' limekuwa chachu kwa Wanahiphop wengi kujiita mfano,leo tuna NASH MC,P THE MC na wengine wengi pia,lakini athari hizi haziishii tu katika majina bali athari kwa Waghanaji wengi wanaomkubali na kumuelewa Melle Mel,mfano hapa. Nash MC anasema ''Melle Mel ni mtu wa kwanza kudondosha mistari mitamu,ule utamu wa mistari umeanzia kwa huyu mtu''. Hivyo sasa nakumbuka usemi usemao mwisho wa kizuri cha leo ni mwanzo wa kizuri cha kesho,ndugu zangu katika utamaduni huu naomba niwaache mkiperuzi haa machache niliyowaandaleni,AMANI KWENU. (shukrani,(REJEA,Hanzi,M.S,Chuo Kikuu Cha HipHop(2012),Ubunifu Wetu Printing Press,Dar Es Salaam)uk,54,56 na 58. WAKO,Amri Mlela/Niite Maalim (0654 30 40 30).
Thursday, September 12, 2013
Monday, September 9, 2013
MHADHARA WA HIPHOP....MHADHARA WA HIP HOP....MHADHARA WA HIPHOP
JIFUNZE MENGI KUHUSU HIPHOP ---- kupitia blogu hii nashemcee.blogspot.com
Monday, March 25, 2013
HIP HOP VYUONI.
TAZAMA BAADHI YA PICHA ZA MHADHARA WA ELIMU KUHUSU HISTORIA YA HIP HOP NA UHALISIA WAKE ULIOFANYIKA KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA JANA (U DOM)..WATU WENGI WALIJITOKEZA NA ILIKUA NI SIKU YA HISTORIA SANA!! MHADHIRI NASHIR ALIKUA NA JUKUMU LA KUENDESHA MHADHARA HUO AMBAO ULICHUKUA ZAIDI YA SAA 4!! NITAPITA KILA CHUO KUHAKIKISHA ELIMU JUU YA UTAMADUNI WA HIP HOP UNASAMBAA IPASAVYO!! MUNGU TUBARIKI!!
Tuesday, December 11, 2012
Friday, December 7, 2012
UZINDUZI WA SANTURI NNE (04) KUTOKA TAMADUNIMUZIK.
Uzinduzi wa santuri nne (04) kutoka Tamadunimuzik mnamo tarehe 08/12/12 pale New Msasani Club kwa kiingilio cha elfu tano tu njoo upate raha ya HIP HOP kutoka Tamadunimuzik. Santuri ya KAD GO, AZMA, MANSU-LI, na MUJWAHUKI zitazinduliwa kwa pamoja. Karibu wewe mpenda HIP HOP uje uunge mkono na uendeleze harakati na mapinduzi ya HIP HOP.
Friday, November 30, 2012
UZINDUZI WA SANTURI NNE (04) KUTOKA TAMADUNIMUZIK
Tarehe 08/12/2012 kutakuwa na uzinduzi wa santuri nne kwa pamoja kutoka TAMADUNIMUZIK ndani ya #New Msasani Club kwa kiingilio cha shilingi elfu tano (5000/=) tu getini.
KINA KIREFU | TOLEO LA KWANZA LA MUJAHUKI | JOIN THE REVOLUTION | LOVE STORIES |. HII SIO YA KUKOSA MTAMADUNI NA MPENDA HIP HOP.