Pages

Saturday, March 8, 2014

NASH MC ATOA TAARIFA KWA UMMA: KUHUSU SANAA NCHINI NA HALI HALISI YA MAPOKEO YA KIBAO "KAKA SUMA".

TAARIFA KWA UMMA:Ilikuwa ni siku ya tarehe 7 - 3 - 2014, ambapo katika kurasa pembuzi za mitandao mbalimbali, na taarifa za habari toka vituo mbalimbali vya matangazo nchini Tanzania, ilisikika kuwa "mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) imetoa onyo kwa kituo cha Redio Free Afrca (RFA) baada ya kuwa wamecheza wimbo wa msanii Nash Mc uitwao "KAKA SUMA", wakidai kuwa ni kinyume cha sheria za utangazaji na kwamba kufanya hivyo ni "UCHOCHEZI" uliofanywa na redio hiyo.
Taarifa ambazo Nash Mc alizopokea na hatimaye akapata wasaa wa kusema haya yafutayo;
"Binafsi naendelea kusikitishwa na mambo mengi hapa nchini, likiwemo na hili la TCRA.Wimbo huo uliotoka mwaka jana kati ya mwezi wa 6 na wa 7, ulichezwa katika vituo mbalimbali vya redio nchini na umefikisha ujumbe kwa 100% pasi na shaka, kuendelea kutujengea hofu kwa kusema ukweli ndio chanzo cha uvunjifu wa amani. Ikumbukwe kuwa kila mtu ana uhuru wa kutoa na kupokea habari bila ya kuingiliwa kwa mujibu wa katiba ya sasa, na ndiyo maana vyombo vya habari vinanyimwa uhuru kwa mchakato wa sasa wa kuelekea kupata katiba mpya. Nawakumbusha ,hii ni sanaa na ndio kazi kubwa ya "HIP HOP" na ndio njia sahihi ya kufikisha ujumbe kwa jamii sasa nashangazwa na sentesi ya uvunjifu wa amani.
Ukweli siku zote una nguvu na unapingwa vikali. Yanayoendelea bungeni ni udumishaji wa amani?.Mafisadi wanaokamatwa ni udumishaji wa amani?. Mauwaji ya tembo na biashara za dawa za kulevya zinazohusisha vigogo ni udumishaji wa amani?. Je ni kweli hakuna nyimbo zinazochochea mambo maovu na mabaya nchini zaidi ya KAKA SUMA?. Bora kufa umesimama kuliko kuishi kwa kupiga magoti. Nasubiri kusikia tena wimbo wa Nash Mc uitwao "NAANDIKA" ukifungiwa pia. Wabillahi Tawfiq!".
Hii ni kauli ya msanii Nash Mc, kama alivyotoa taarifa kwa umma (mashabiki wake) kuhusu kufungiwa kuchezwa kwa kibao chake, kwa tuhuma za kuwa kinachochea uvunjifu wa amani, lakini mashabiki, wataalamu wa sanaa, wanataaluma mbalimbali wanabaki wakihoji suala la kufungiwa kwa kibao hiki kuwa wamezingatia vigezo gani, na kuacha maswali kadhaa ikiwemo. 1. Je, mamlaka inatambua ni ipi dhima ya fasihi/sanaa katika jamii.
2. Wanahakiki kazi za msanii kwa kutumia vigezo gani?.
3.Je, katiba imefuatwa vyema hapo?, hasa ile ibara ya 18, SURA YA KWANZA, SEHEMU YA TATU?.
Hayo ni baadhi ya maswali toka kwa wataalamu wa sanaa, mashabiki n.k, sasa ni jukumu lako shabiki kutafuta kibao hiko na kukipitia kwa jicho la kihakiki, ili ubaini kinachoongelewa, , upendo mmoja, amani itawale, AKHSANTE
Mwanazuoni, 2014 (muendesha blogu).

5 comments:

  1. SIRI KUBWA AMBAYO VIONGOZI WETU HUTUMIA KUTUNYANYASA, KUTUNYONYA, KUTUONGOZA MIAKA NA MIAKA NI KUTUNYIMA ELIMU NA UFAHAMU JUU YA MAMBO YANAYOENDELEA KILA SIKU! WANATUZUGA WANATUPENDA KUMBE WANATUKANDAMIZA KWA KUKOSA UFAHAMU NA UJUZI WA KUCHAMBUA MAMBO!
    SO UMEKUJA MAAALIM NASH, UKAIZINDUA MITAA, KWA MAPENDO YAKO NA JAMII, KWA MBINU ZA LUGHA, UKIONGOZWA NA MZIMU WA SHAABAN ROBERT, KUPIGANA HII VITA, NA KUANDIKA, TABIA YA KAKA SUMA YA KUTUKANDAMIZA HADI HOMA ZINATUZIDIA KAMA TUMEAMBUKIZWA NA VVU. "SO KITENDO CHA KUIZINDUA MITAA HAWATAKI THUS Y" ILA WAO SIO MUNGU TUNAKUSAPORT NA NGOMA TUNAISIKILIZA HAWAWEZI KUITOA JAMII, HAWAJIFUNZI MTWARA. LOVE & PEACE LONG LIVE BRODAH!

    ReplyDelete
  2. WANATAKA TUSIKILIZE BABY BABY I LOVE YOU ILI ZITUHALIBU UBONGO TUSIWE TUNAFIKIRIA MAISHA NA UNYANYASAJI WAO ILA TUFIKIRIE MAPENZI TU PUMBAVU ZAO!
    AFU SIWAPENDI KINYAMA MBONA KUNA NYIMBO NYINGI TU ZINAZOHARIBU TAMADUNI ZETU HAZIFUNGIWI Y ALWAYS HIPHOP MUSIC???

    ReplyDelete
  3. hawana lolote hao
    ngoma inaelekea kufunga nusu mwaka leo wanazingua.mi siku zote nasema
    dawa ni kuwaandama maana hii ya kudai haki zetu kwenye mitandao tu
    haitosh inabid wizara husika iwe inawajibika kila linapotokea swala
    kama hili.



    swahili rap

    ReplyDelete
  4. @jesey, sanaa ni akiso la jamii hivyo haiwezi zingwa isiangaze yajiriyo kwenye jamii.

    ReplyDelete
  5. @ze kitab, kazi ya sanaa ni kuelimisha, kufundisha, kukosoa, na kuadibu, sasa kama hayo yasingekuwepo kusingekuwa na tawi/kazi hii ya sanaa

    ReplyDelete