Oi, oi, oi, kama ilivyoada utamaduni wa Hiphop unavyotulea katika misingi yake ELIMU NA BURUDANI, basi nasi hatuna budi kutomuangusha mlezi huyu, leo katika blogu letu makini kabisa, kuna hili, NASH MC, baada ya kuachia kibao chake "naandika",mwanzoni mwa mwaka huu na kupokelewa vizuri na wanajamii (Wapenzi wa HipHop. Sasa yuko jikoni akijiandaa kutoka na "EP", yaani "Extended Play", mmmh!, " EP", ndo, nini sasa?, waweza jiuliza ukabaki na uvulivuli katika hili, ila hapa tutaelezana, dhana hii inanikumbusha kipindi THORIA alivyoachia kazi zake zake za mwanzo kabisa katika mfumo huu, hivyo sasa "EP", ni demo album (santuri) yenye nusu nyimbo zitakazokua kwenye album(santuri) ni kama trailor tracks (vionjo) vya albam inayokuja, wakati mwingine watu wanatoa ili wawape mashabiki kitu cha kuwa weka katika umakini kabla album (santuri) kamili haijatoka, na inakuwa na nyimbo mpaka 7, hivyo sasa Nash anawaambia mashabiki wake wakae mkao wa kupata kazi hii, endelea kutembelea www.nasheemcee.blogspt.com, waambie na wale pia, HipHop Kwa Maisha.
Pages
▼
No comments:
Post a Comment