Pages
▼
Thursday, September 12, 2013
JE NASH EMCEE ANAIZUNGUMZIAJE MITINDO HURU?
Ndugu wadau,wakereketwa au wanunuzi wa kazi zetu za HIPHOP
na wote wanaotoa mchango wa hali na mali katika kuhakikisha
gurudumu la sanaa hii linateleza kama tutakavyoona inafaa..
Leo katika blogu yetu hii ndugu wasomaji na wadau wake
tuna kijimada hapo kama kinavyosomeka hapo juu...
Nash Emcee alipata fursa ya kuzungumzia jambo hili ambalo
limeonekana kukanganya mbongo za sisi wafatiliaji kwa kujua
kuwa mitindo huru au FREE STYLES ni katika nguzo za HIPHOP
hivyo sasa Nash anajaribu elezea suala hili kama inavyoonekana
hapa chini,karibu....
"Bongo (Tanzania)watu wamejaribu kuingiza
mitindo huru kama nguzo ya Hiphop,hakuna freestyle ''mitindo huru''
kama nguzo ya HipHop lazima uwe unajua kughani ndipo uweze kufanya
mitindo huru,hiyo ni kama binzari (kinogeshaji)tu katika ughanaji"
Katika hali halisi tu,hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kufanya mitindo
huru ya HipHop bila kughani.Mitindo huru ni moja kati ya vipande/kijisehemu
kinachounda nguzo ya ughanaji(EMCEEING)....
Ndugu msomaji katika hili na katika kile kinachosisitizwa kuwa
Mwanahiphop anahitaji tafuta maarifa (knowledge) katika mambo
mbalimbali yanayomzunguka hata pia katika utamaduni wake,natumai
ntakua nimejaribu rahisiha hilo katika kupeana maarifa,Amani Kwenu.
(shukrani_(REJEA,Hanzi,M.S,Chuo Kikuu Cha HipHop(2012),Ubunifu Wetu Printing Press,Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment